CHANZO: JAMII FORUM
Kauli za Dk. Slaa zimekuja baada ya Mchungaji Gwajima kujitokeza kwenye media na kudai hakuwahi kuwa mfuasi wa Lowassa bali ni mfuasi wa mabadiliko ya nchi na siyo mfuasi wa mtu au personality ya mtu.
Ikumbukwe Dk. Slaa aliamua kuwa mkimya katika kipindi ambacho taifa likikuwa katika harakati za kampeni za Uchaguzi Mkuu.
Dk. Slaa ameyasema haya kupitia akaunti yake rasmi (verified user) ya Jamiiforums.
Dk. Slaa amesema,
Ndiyo maana siku chache zilizopita nilisema:
i) Ni muhimu kwa "Mshenga Gwajima" kutubu na kuwaomba Radhi Watanzania kuliko kuendelea kuwapotosha.
ii) Mungu hamilikiwi na binadamu awaye yote. Watanzania tunawajibu wa kumshukuru sana Mungu kwa kutukomboa na kutuokoa na " Mabadiliko" ya " Kuzungusha Mikono". Mshenga na UKAWA yake walitaka kutuaminisha sote kuwa Mabadiliko ni kuzungusha mikono! Walitaka kutuaminisha kuwa "Mabadiliko ni Lowassa na Lowassa ni Mabadiliko".
Lowassa aligeuzwa kuwa "Ajenda" badala ya ajenda za Msingi za Wananchi. Mungu amesikiliza Sala za Wanyonge na Walalahoi. Namshukuru sana Mungu aliyenionyesha kuwa kati ya wawili hao, japo wote kila mmoja ana uchafu, Magufuli ni "Nafuu mara eflu" kuliko fisadi Lowassa. Asante sana Mungu Mwema kwa kulinusuru Taifa lako lililotaka kuingizwa "mjini" na makuwadi kwa ulaghai na upotoshwaji uliopitiliza.
iii) Nilimtaka Gwajima awaombe radhi Maaskofu aliosema "wamehongwa na Lowassa na kuwa fedha hizo waligawiwa mbele ya Mavho yake. Alisema bila kumumunya maneno, kuwa.... Maaskofu wa ki lutheri alikwisha malizana nao" na kuwa kati ya "Maaskofu wa Kikatoliki 34 wamehongwa Maaskofu 30 na kumtaja kwa jina Askofu Mkuu mmoja, ambaye yeye kapewa fedha za kununulia gari la kiaskofu." Fedha hizo alidai zimetolewa na Lowassa kupitia Rostam Azizi. Gwajima, Tambua kuwa kama ni kweli toka tena hadharani wakemee Maaskofu wanaopokea Rushwa, na kama si kweli Waombe Radhi hadharani Maaskofu hao kwani kauli hiyo ilitaka kuwagawa Maakofu na kuwachafua
Lakini, alitamka hayo akiona ni sifa, ndiyo maana nilimshangaa kiongozi wa dini ambaye badala ya kukemea anaona ni sawa. Kama wenzangu waliokuwepo na wao wana Misingi ya kusimamia basi watatoa ukweli wao, na kama wanachukia ufisadi basi watatoka hadharani kukemea tamko hilo lililotolewa mbele yetu watu 4 akiwemo Mshenga.
Nilipotamka hivi wengi walidhani Dr. Slaa ndiye Katamka kuwa Maaskofu "Wamehongwa". Kama Askofu anaweza kufika mahali akawasingizia wenzake ni hatari sana na halihitsji kufungiwa Macho na masikio. Kama anavyosema Gwajima ni "kweli". Basi wote tunaopenda kupiga vita Ufisadi ni lazima tupaze sauti zetu, na kukemea kitendo hicho kama kweli kimefanywa na wale tunaotegemea kusimamia maadili katika Jamii yetu. Wako walioniambia Dr. Slaa unapata wapi ujasiri wa kuwasema viongozi wa dini. Sijawahi kuyumba wala kuyumbishwa. Ukweli utatamkwa hata kama ni mchungu, na uovu na uozo utasemwa tu hata kama umetendwa na nani. Ukitazama nyuso za wazi " haki haitatendeka milele.
iv) Katika busara ya kawaida, hatukutegemea Gwajima kujitokeza "Kumkana Lowassa" hasa kabla ya kuomba radhi. Aidha Kauli " Live" kwenye YouTube na mitandao mbalimbali ziko bado kibao. Ama kweli Gwajima ni kiongozi asiye na dhamira kukanusha kauli zake hizo kabla ya kuomba radhi.
v) Wako watakaodhani kuwa Dr Slaa ana "bifu" binafsi na Gwajima. Ni kweli kibinadamu nimeumia sana kwa kuwa kuumizwa na rafiki kunaumiza sana, lakini nawaonea huruma zaidi Watanzania Waliobebwa kwa ushabiki mkubwa na kupoteza nguvu zao nyingi na labda "kupoteza fursa ya kuiondoa CCM kwa muda mrefu ujao" kwa kuwaamini watu kama kina Gwajima. Hiki ndicho kinachonisukuma zaidi kuendelea kumkaba Gwajima hadi atakapoomba radhi kwa watanzania wanyofu.
Nawaomba Watanzania tuwe na kumbukumbu. Tuzisikilize tena Kauli mbalimbali alizozitoa Gwajima, tena wakati mwingine kwa njia ya Maombi kwa jina la Mungu. Hali hii isipokemewa kwa ukali sana ni hatari sana.
Ndugu zangu wanaJF na Watanzania wote,
Pamoja na yote haya, ninawatakia Heri nyingi kwa sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2016 uwe wa Baraka na mafanikio.
Baadhi ya wanaJF wakataka kufahamu zaidi kuhusu kauli yake. Mmojawapo alimuuliza swali hili,
- Kamanda,
Naona hujalala saa hizi! Msimamo wangu ulikuwa wazi. Mshenga alikuja kwangu kunijulisha yaliyotokea Dodoma na kunitaka tuone namna ya kumpokea. Nikampeleka kwa Mwenyekiti wa Chama. Hiyo ndiyo "Mimi kuanzisha mchakato". Nimeeleza mara kadhaa lakini naona watu wameshindwa kupambanua.
Nilieleza kuwa nilishiriki majadiliano ya Kumpokea Lowassa. Tofauti ya mimi na wenzangu ni kuwa niliweka Masharti kama Katibu Mkuu ili kukilinda Chama changu. Moja ya Sharti ni kutaka kujua kama Lowassa ni "Asset au ni Liability". Hadi tarehe 27/8 hoja hizo zikawa hazijajibiwa na nikaona wenzangu tayari wamefikia uamuzi wa kumpokea bila kuangalia athari kwa CHADEMA.
Kama mwanademokrasia, Wengi wakifikia uamuzi wewe ambaye hukubaliani nao ndio unakaa pembeni. That is what I did Kamanda.
Motion kama unavyoita wewe ilianzishwa na Mshenga siyo na mimi. Japo taarifa ninazopata sasa ni kuwa move hiyo ilikuwepo mapema hata kabla mshenga hajanifikishia. Inasemekana kuja kwangu ilikuwa changa la macho tu kwa lugha ya siku hizi. Taarifa nyingi ndiyo zinaanza kupatikana sasa, nisingelipenda kuzizungumzia kabla sijazichambua vizuri.
No comments:
Post a Comment