Wema Sepetu alizaliwa tarehe 28, September, ni mtoto wa
mwisho kati ya mabinti wanne wa Mzee Sepetu.
Wema hakufikiria kama atakuja kuwa mmoja kati ya ma-star
wakubwa hapa nchini hadi nchi za nje mpaka siku mmoja alipo kuwa kwenye
matembezi yake Slypway Masaki alikutana na dada Mange Kimambi na kushawishiwa
ashiriki mashindano ya Miss Tanzania 2006...
Wema Sepetu aliibuka
kidedea na kuwagalagaza Jokate Kidoti Mwegelo na Lisa Jensen
Kabla ya kuwa miss Tanzania alikuwa na mwandani wake japo
hakuwa super star lakini hawakudumu maana aliposhikilia taji alikuwa busy jambo
lililomfanya akose muda wa kumpa mwandani wake lakini muda mchache akakutana na
Marehemu Kanumba na kuanza uhusiano mara moja....
Uhusiano baina ya Kanumba na Wema ulikwenda vizuri sana
nakama mchezo nyota zao zote zikang'aa sana Kanumba sasa akaonekana Kanumba
kweli si yule wa kwenye maigizo ya kikundi cha Kaole tena uhuu ni ukweli
kabisa.. na haswa waliposhirikiana katika movies zao walizidisha umaarufu mara
dufu, lakini kiukweli ni kwamba Kanumba ndiye aliye gundua kipaji cha Wema na
ndiyo aliye muibua katika sanaa ya kuigiza.
Wema sijui ni utundu au utoto au ulimbukeni wa mapenzi basi
akamsaliti Marehemu Kanumba na kuwa na mvuta bangi Jumbe.
Pichani ni Wema na
mpenzi wake Steven Kanumba enzi za uhai wake Kanumba (RIP)
Kwakweli katika mapenzi yote nazani alipochemsha binti wa
Sepetu ni pale alipokuwa na Jumbe maana ilimpelekea hadi kuwekwa rumande.
Natusinge angalia Wema naye angekuwa mvutaji bangi na madawa ya kulevya
Wema mahakamani akiwa na mpenziwake wa zamani Jumbe
Wazazi wake haswa mama mtu alijitahidi sana kumuokoa Wema
kwenye mikono mibaya ya Jumbe
Heka heka za Wema wa
Sepetu hazikuishia hapo akajikuta mikononi mwa Chalz Baba kaka yangu na mie
huyooo
Wazazi wakaona basi
tena maana mwanao kutwa magazetini wakampeleka Ulayaaaa...sasa akiwa marekani
kwa mmoja wa dadazake huko alikuwa anachati na watu kwa kutumia mitandao ya
kijamii hii chating ya kwanza ya Wema na Diamond ilikuwa kwenye FACEBOOK siku
hiyo mtoto wema alikuwa anacomment kwenye wall ya Diamond kimahaba huku mtoto
wa mbagala akijibu mashambulizi asije poteza bahati
Mara Wema anasema mtu kifudenge naona kachoka a reply sasa
hivi ....ikitajwa hivyo Diamond ana jibu akijijua yeye ndio mtukifudenge
Dah! enzi hizo diamond alikuwa kituko jamani hajulikani
kabisaaaa watu mkisikia wimbo mkali wa mbagala mnatafuta aliyeimba nani mnakuta
kituko mnabakia lakini anaimba vizuri.
Wema Sepetu alipotua tu inchini alifikia kupanga na
kumkaribisha mpenzi wake mpya Diamond na kuanza maisha ya pamoja ya raha na
mstarehe.....
Kwakweli watanzania wengi walipigwa na butwaa kila mmoja
alilalama why Wema akachukua kinyarika kama hicho na mengi mabaya juu yao.
Nausifu sana ujasiri wa Wema kwani aliweka pamba masikioni
na kutaka kutudhihirishia kuwa Naseeb aliyempenda yeye ni Almasi ...Diamond
ambayo inang'aa duniani kote.
Hapa tunaona kabisa japo Diamond Platnum alishatoka na
nyimbo zake kama mbili hivi kali moja wako ya Mbagala lakini hakuwa juu kiasi
hicho na bila Wema angebakia kama wasanii wengine wanatesa na nyimbo kali ila
nyota hazing'ai kivileee Ben Pol, Chid Benzi Barnaba na wengineo.
Wema hakuona haya kumpenda hadharani Diamond alimpiga mabusu
hadharani watu wakapaka sana domo na mengineyo mengi lakini alizidisha mapenzi
mara dufu. Ndipo tukaanza kumuona Diamond muonekano wa pili aling'aa sana akawa
na swaga za Wema, kiingereza kidogo kila mwanamke akatamani awe kama Wema na
Diamond wakawa hadithi tamu midomoni mwa watu navile mtoto Wema anavyojua
kudeka na kupenda watu wakachanganyikiwa na mapenzi yao yalivyo noga.
Tutashangaa sana kwanini awali watu hawakupenda na wengine
walimcheka sana Wema kuwa na Diamond lakini sasa jamii nzima inataka kusikia
kwamba Wema amerudiana na Diamond...umeona eheee?
Mtu wa karibu na madam alininyetisha kwamba Wema alimpenda
kwa dhati Diamond japo alipigwa vita sana na jamii kuwa hafai na si wa hadhi
yake lakini hakuvunjika moyo alimpenda zaidi Diamond nakutufanya watanzania
wote na ulimwengu wote kumtambua Diamond na kipaji chake na hadi tukamuona
handsome wakati alikuwa hatazamaniki eti leo hii amekuwa super star anajidai
kumbwaga na kumsaliti tena na kutembea na mashoga wa Wema kwakweli hii haijakaa
sawa kabisa..hatuwezi kuwaacha walale na huyo kinyago wake Penny asiye kuwa
hata na aibu namshangaa bado analazwa kwenye mashuka ya Wema na anakubali
kwanini kama anampenda asimletee mengine wakalala ndio tuwaache..Diamond ni wa
Wema tu labda arudie ule uchokoraa wake wa zamani wa mbagala ndio tutamucha
sasa nao wamchukue wamng'aishe tuone kama watamgombea tena alisema kwa huzuni
mnyetishaji.
Wema Sepetu
amezidi kupata umaarufu japo magazeti mengi yakiendelea kumchafua usiku na
mchana lakini ni binti ambaye aseme leo atakuwa jangwani anayetaka kumuona aje
basi hakika maelfu ya watu watakusanyika hapo nyota yake kwakweli iko juu mno
ndio mana kila atakaye mshika mkono naye lazima awe juu na hii si kwa wanaume
wake ni hata mashoga zake wa kike mfano halisi ni Snura.
Pamoja na Wema
kusemwa sana magazetini na kusalitiwa mara nyingi na kusemwa vibaya na mashoga
zake na yote hayo lakini bado yuko juu kwani binti huyu ana kampuni yake ya
production inayoitwa Endless fame na bado anakipindi chake ambacho hivi
karibuni kinategemewa kurushwa hewani kitakachoitwa Reality Show na anajiweza
imaisha na Mungu anazidi kumbariki kwani anajitoa sana kwa watu na sadaka,
anamiliki nyumba na magari kwakweli Wema Sepetu you shine like diamond... your
a star isiyo fifia.
Ombi kwa dada Wema ni kwamba achana na Diamond hakufai
anataka kukumaliza tu ili akae pembeni akucheke anatambua kabisa ulimwengu
mzima wote unajua ameng'ara kwa kupitia nyota ya Wema sasa anataka akuzime ili
apate kutawala yeye achana naye bwana fanya ya maendeleo atakutafuta mwenyewe
kwanza mnapo weka story kila siku Wema na Diamond ndio unamsaidia auze kazi
zake maana akitoa nyimbo kila mmoja anataka ajue safari hii anamwimbia nini
Wema yaani hauzi bila ya jina lako kama umemshtukia akiwa anatoa album au wimbo
ndio zinakuja skendo za Wema na Diamond inamaana ndio muda huo huo anapo
tafutia skendo auze yeye kwa kukupitia mgongo wako.
No comments:
Post a Comment