Translate

Monday, August 22, 2016

MAWAZIRI WAPEWA SIKU 21 ZA KUHAMIA DODOMA





MAWAZIRI wa wizara mbalimbali, wanapaswa kuhamia Dodoma, ndani ya wiki tatu baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuhamia.Waziri Mkuu alishatangaza kuwa atakuwa amehamia ifikapo Septemba, mwaka huu.

Mawaziri hao ambao wameshatajwa kwa majina, wanapaswa kuhamia Dodoma ndani wiki mbili hadi tatu baada ya Majaliwa kuhamia Dodoma.majaliwaKutokana na taarifa hiyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk Charles Tizeba ambaye alishatangaza kuhamia Dodoma akiwa waziri wa kwanza kutoa kauli hiyo baada ya Waziri Mkuu, alisema jana kuwa wameshapokea maagizo. Tizeba alisema kwamba ndani ya wiki mbili hadi tatu, baada ya Waziri Mkuu kuhama, nao wanapaswa wawe wameshafika.

Kwa upande wake, Kaimu MseMaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja, alisema wizara hiyo imejipanga kuhamia Dodoma na kwamba wanachosubiri ni utekelezaji wa kwenda huko.

Wakati wizara hizo mbili, zikiwa tayari kwa kuelekea Dodoma, nayo Wizara ya Nishati na Madini kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Profesa Justin Ntalikwa imesema maelekezo kwa wakuu wa idara na vitengo wote, yameshatolewa ili kufanya maandalizi kwa ajili ya kuhamia Dodoma ifikapo Septemba mwaka huu

No comments:

Post a Comment