Mwanafunzi mmoja nchini Brazil ameshea picha mbalimbali akiwa kitandani na Usain Bolt.Jardy Duarte, 20, alipost picha kwenye group la WhatsApp akiwa na nguli huyo wa riadha wakipena mabusu na kukumbatiana.Kwenye moja ya picha walizopiga Bolt ameonekana akimkumbatia Jaddy kwa nyuma, akiwa amevaa vest nyeupe, huku nyingine akionekana kumbusu shavuni.Picha hizo zilisambazwa na mwanafunzi huyo wa Brazil na zimeonekana kwenye baadhi ya vyombo vya habari nchini kwake ikiwa ni pamoja na El Globo.Bolt ambaye jana alifikisha umri wa miaka 30, alisherehekea mpaka asubuhi kwenye klabu ya usiku ya Barra de Tijuca iliyopo Rio.
Mkimbiaji huyo wa mbio fupi wa Jamaica ameweka historia kwa kushinda medali tatu za dhahabu kwenye michuano mitatu mfulululizo (tripple-tripple) kwenye mbio za mita 100, 200 na 4×100 (za kupkezana vijiti).
Jady, ambaye pia alikuwa maeneo ya Rio, ameelezea namna gani Bolt alivyotumia walinzi kumpata.
“Aliwatuma walinzi waje kuniita. Lakini kwa wakati ule sikufahamu hata kama alikuwa ni yeye, kwasababu walikuwa Wajamaica wengi sana.”
“Halikuwa jambo la kushangaza saaana. Ilikuwa kawaida tu.
“Nilituma picha hizo kwenye group lawasichana wenzangu wa shuleni na kusema ‘yeyote ambaye alifuatilia Michuano ya Olimpiki basi lazima atamjua huyu’.”
Hata hivyo dada yake Bolt, Christine Bolt-Hylton, 32, amefichua kwamba, mdogo wake yuko kwenye mahusiano ya muda mrefu na mrembo wa Kijamaica Kasi Bennett.
No comments:
Post a Comment