Translate

Thursday, August 11, 2016

WAZIRI NAPE ATOA TAADHARI KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU UCHOCHEZI

  


Waziri wa Habari, Utamaduni. Sanaa na Michezo nchini, Nape Moses Nnauye ametoa tahadhari kwa waandishi na vyombo vya habari ambavyo vitajihusisha na kuripoti mikutano, maandamano au habari yoyote ambayo ni ya kichochezi kwa taifa kuwa vitahesabika kuwa vyenyewe navyo ni vya kichochezi, hivyo
chombo husika kinaweza kufungiwa kwa kueneza uchochezi.
Amesema vyombo vya habari havipaswi kuripoti habari za kuonyesha kuichonganisha serikali na wananchi wake.
Hayo yamesemwa wakati wa kumtambulisha ndugu Hassani Abbas aliyechukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Habari-Ikulu (Msemaji wa Serikali), Assah Mwambene.



Chanzo: Magic Fm

No comments:

Post a Comment