Translate

Thursday, July 13, 2017

CHADEMA GEITA YAWAVUA UANACHAMA VIONGOZI WAKE WAWILI



 cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoani Geita kimewafukuza na kuwavua uanachama viongozi wawili huku kikitoa onyo kwa wanachama wake kwa kuhusishwa na kashifa ya usaliti na kuhujumu Chama hicho
. Katibu wa Chadema Jimbo la Geita mjini Kangeta Ismail amesema wanachama wake waliofukuzwa ni Edward Manyika ambaye alikuwa katibu mwenezi wa jimbo hilo na Daud Sunzu aliyekuwa mgombea Udiwani kata ya Kalangalala katika uchaguzi mkuu uliopita. Amesema kufukuzwa kwa wanachama hao kumetokana na maamuzi ya kamati tendaji kupitia kikao cha dharura kilichoketi jana na kwamba wengine watatu wamepangiwa tarehe ya kuwasilisha utetezi wao Kangeta ameendelea kusisitiza kwamba chama hicho kitaendelea kuwachukulia hatua viongozi na wanachama wanaokiuka maadili ya Chama ambayo yamewekwa .

No comments:

Post a Comment