Translate

Tuesday, August 22, 2017

TUNDU LISSU AKAMATWA

TUNDU LISSU

Mbunge wa Singida Mashariki, Waziri Kivuli wa Katiba na Sheria, Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Wakili wa Mahakama Kuu Tanzania na Mwanasheria Mkuu wa Chama cha CHADEMA Mheshimiwa Tundu Lissu, amekamatwa na Mlinzi wa amani alipokuwa anatoka mahakamani Kisutu .


Wamesema wamemkamata kwa ajili ya mahojiano.

"Tumetoka Mahakama ya Kisutu muda huu ambapo Mwanasheria Mkuu wa Chama, Tundu Lissu alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi (uchochezi one) lakini pia alikuwa ni wakili kwenye kesi inayomkabili Yericko Nyerere hapa hapa Kisutu.

Wakati gari la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likawa blocked na nyuma ya gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na atakiwa kwenda Central Police.

Wakamtaka ashuke kwenye gari lake na apande gari jingine la kwao kwa ajili ya kuelekea Central Police".
 Amesema Makene.

CHANZO :JAMII FORUM

No comments:

Post a Comment