Translate

Saturday, September 2, 2017

RUTO ATAKA TAREHE MPYA YA UCHAGUZI KUTANGAZWA KENYA.



Naibu rais wa Kenya , William Ruto, ameiambia tume ya uchaguzi ya Kenya kutaja rasmi siku ya kurudiwa kwa uchaguzi wa urais nchini humo.

Hii ni baada ya hatua ya Ijumaa ya mahakama ya juu zaidi kubatilisha ushindi wa Rais Uhuru Kenyatta , wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi uliopita , ikisema kulikuwa na dosari kubwa zilizokiuka katiba ya Kenya.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga aliyeusifu uamuzi huo wa mahakama, papo hapo alishtumu vikali tume ya uchaguzi ya Kenya IEBC na pia kuwalaumu waangalizi wa kumataifa kwa kile alichokitaja ' kuhalalisha udanganyifu uliotokea na kutaka uchunguzi zaidi ufanyike.
Mahakama yafutilia mbali ushindi wa Kenyatta
Amewataka waliohusishwa na udanganyifu huo kujiuzulu , kufutwa kazi na hata kuchukuliwa hatua za kisheria wakisema kamwe hawawezi kuaminiwa kusimamia uchaguzi ujao.
Kwa upande wake Rais Uhuru Kenyatta amesema japo anauhesimu hakubaliani na uamuzi huo uliofutilia mbali ushindi wake na kwamba yuko tayari kwa marudio ya uchaguzi huo unaotakiwa kufanyika katika kipindi cha miezi miwili ijayo.

No comments:

Post a Comment