Translate

Saturday, August 29, 2015

TRENI ILIYOPOTEA NA SHEHENA YA DHAHABU MIAKA 70 ILIYOPITA YAPATIKANA!

Afisa mmoja wa serikali ya Poland, amesema kuwa ana imani kuwa treni moja ya kijeshi ambayo imefichwa tangu vita vya pili vya dunia, zaidi ya miaka sababini iliyopita, na kusemekana kubeba vitu vya dhamani, imepatikana, chini ya ardhi Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.

Naibu waziri wa utamaduni amesema shehena iliyoko kwenye treni hiyo bado haijulikani. Kwa mujibu wa ripoti treni hiyo ilipotea ikiwa imejaa shehena ya dhahabu kutoka mji wa Breslau nchini Ujerumani, mji ambao kwa sasa unajulikana kama Wroclaw and sehemu zingine za Poland, wakati wanajeshi wa Ujerumani walipokaribi mji huo. Afisa mkuu wa makavazi ya kitaifa, Piotr Zuchowski, amesema anaimani kuwa treni hiyo itapatikana chini ya ardi karibu na mji wa Walbrzych.

Amesema ameona picha zilizopigwa na kifaa maalum chini ya ardhi ikionyesga treni hiyo yenye urefu wa karibu mita mia moja ikiwa na bunduki juu yake. Amesema hamna anayefahamu kile treni hiyo ilikuwa imebeba wakati huo na asema anatarajia iwe na vitu vya Sanaa vilivyoibiwa nchini Ujerumani wakati wa utawala wa Kinazi. Raia wawili ambao hawajatambuliwa kutoka Ujerumani na Poland waliifahamisha utawala wa eneo hilo kuwa wanafahamu eneo lililofichwa treni hiyo, na wamedai wapewe asilimia kumi ya vitu vitakavyopatikana ndani yake. Watu hao wanasema kuwa walipewa habari hizo na mtu mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa walioficha treni hiyo, muda mfupi tu kabla ya mtu huyo kufariki.

No comments:

Post a Comment