Translate

Wednesday, January 27, 2016

CHENGE ALIVURUGA BUNGE JIONI HII

Taarifa za muda huu kutoka Dodoma.........
.Wabunge wa kambi ya upinzani wameondoshwa ndani ya bunge jioni hii,hii inafuatia mwenyekiti wa bunge Mh Andrew Chenge kuamuru baadhi ya wabunge watolewe nje kwa kukaidi amri ya mwenyekiti ya kuwataka kukaa chini,miongoni mwa waliotakiwa kutolewa ni Tundu Lissu(mnadhimu mkuu wa kambi ya upinzani.)
Tangazo la kuwatoa nje wabunge wa upinzani lilipingwa na wabunge wa upinzani walioamuua kuendelea kusimama huku wakiwa wameshikana mikono,uamuzi huo wa wabunge kushikana mikono ili kuzuia wenzao kuondoshwa nje kulisababisha mwenyekiti wa wabunge kuamuru askari wa bunge kuingia ndani na kuwatoa wabunge wote wa kambi ya upinzani,bunge linaendelea bila wabunge wa upinzani
ambao wametoka nje.

No comments:

Post a Comment