Live kutoka Dodoma usiku huu...
Nape amesema sababu ya kuzuia TBC kurusha bunge lote live ni zifuatazo.
1.Gharama za kuendesha matangazo ya live ni kubwa,kwa mwaka TBC wanatumia bilion 4.2,huo ni mzigo mkubwa.Anasema TBC kutokana na kukumbwa na ufinyu wa bajeti,ilikuwa kidogo washindwe kurusha vikao vya sasa vya bungE
2.Watu wengi hususani watumishi wa umma,badala ya kufanya kazi wao wamekuwa wanakalia kutazama bunge tu,kwa hiyo ili wafanye kazi,serikali imeona bora bunge liwe linarushwa usiku ili mchana watu wafanye kazi.
3.Kuna kundi kubwa sana,kama machinga,mama ntilie na wengine muda bunge linapouwa live wanakosa fursa ya kuona bunge,serikali imeona ili kuongeza idadi ya watazamaji wa bunge ni vema bunge likawa linarekodiwa na kurushwa usiku
4.Nchi nyingi kama India,Uingereza,Sirlanka,Malawi,Lesotho,Sinapour n,k hawaoneshi bunge kwa siku nzima,Nape anasema huu utaratibu wa kurusha bunge upo Tanzania pekee.
No comments:
Post a Comment