Translate

Monday, July 5, 2021

NDEGE ZA ZIMAMOTO ZAPELEKWA KUSAIDIA CYPRUS

Cyprus seeks Israel, EU help to fight wildfire

Umoja wa Ulaya umetuma usaidizi wa angani kusaidia katika kudhibiti moto mkubwa wa msituni unaosambaa katika miji ya kaskazini mwa Cyprus ya Limassol na Larcana.

Mkuu wa Umoja huo pamoja na Tume ya Umoja wa Ulaya, wamesema ndege za kuzima moto zimetoka Ugiriki kwenda kupambana na moto huo ambao maafisa wa Cyprus wanasema ni mbaya zaidi katika rekodi yake.

Italia pia inapanga kupeleka wazima moto wa angani. Waziri mkuu wa Israel Naftali Bennet ameitikia ombi la usaidizi kutoka kwa rais wa Cyprus, Nicos Anastasiades na kusema watatuma ndege zao za wazima moto leo Jumapili.

Moto huo umesababisha uharibifu wa mali, lakini hakuna ripoti zozote za majeruhi. Chanzo cha moto huo ulioanza Jumamosi mchana hakijabainika lakini taifa hilo limesajili ongezeko la kiwango cha joto kupita nyuzi 40 kwenye vipimo vya Celsius. 

No comments:

Post a Comment