Papa Francisko Alazwa Hospitalini Kwa Operesheni Kubwa, Roma!
Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 4 Julai 2021 majira ya jioni amelazwa kwenye Hospitali ya Gemelli iliyoko mjini Roma kwa ajili ya kufanyia operesheni kubwa kwenye utumbo mpana. Operesheni hii inafanywa na Prof. Sergio Alfieri. Baada ya operesheni, Hospitali ya Gemelli itatoa taarifa kuhusu hali ya Baba Mtakatifu Francisko. Jumapili mchana amesali na waamini Angelus
Dk. Matteo Bruni msemaji mkuu wa Vatican amesema kwamba, Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili tarehe 4 Julai 2021 majira ya jioni amelazwa kwenye Hospitali ya Gemelli iliyoko mjini Roma kwa ajili ya kufanyia operesheni kubwa kwenye utumbo mpana. Operesheni hii inafanywa na Prof. Sergio Alfieri. Baada ya operesheni, Hospitali ya Gemelli itatoa taarifa kuhusu hali ya Baba Mtakatifu Francisko. Kabla ya kwenda kufanyiwa operesheni kubwa, Baba Mtakatifu Francisko, Jumapili amesali na kutafakari na waamini pamoja na mahujaji waliofika kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican kuhusu “Kashfa ya Fumbo la Umwilisho”.
Kwa sasa waamini na watu wote wenye mapenzi mema, wanaalikwa kumkumbuka na kumwombea, ili kazi hii ya madaktari ipate kibali na hitimisho lake kwa baraka za Mwenyezi Mungu! Radio Vatican itaendelea kukujuza hali ya Baba Mtakatifu Francisko kadiri taarifa zitakavyokuwa zinatolewa na Hospitali ya Gemelli
No comments:
Post a Comment