SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), imesema imejipanga kuhakikisha Uchaguzi Mkuu wa marudio utakaofanyika Machi 20, mwaka huu unakuwa huru na haki kwa kupambana na makundi ya aina ya watu mbalimbali wanaokusudia kufanya fujo ikiwemo kuwazuia wenye sifa wasipige kura
.
Hayo yalisemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud wakati alipozungumza na watendaji wa Serikali wakiwemo wakuu wa wilaya na mikoa na baadhi ya vikosi vya ulinzi mjini Chake Chake, Pemba.
Alisema zipo taarifa kwamba kipo kikundi cha watu kimeandaliwa kwa ajili ya kufanya vurugu katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu, ikiwemo kuwazuia watu washindwe kwenda kupiga kura kwa malengo ya kisiasa zaidi.
Aboud alisema, Serikali haiwezi kuvumilia watu wa aina hiyo pamoja na vitendo hivyo ambavyo vinakwenda kinyume cha demokrasia ya mfumo wa vyama vingi inayotoa fursa zaidi kwa watu kushiriki katika Uchaguzi Mkuu kwa kuwachagua viongozi wanaowataka.
No comments:
Post a Comment