Translate

Thursday, January 28, 2016

STAA KAJALA AFUNGUKA MAZITO KUHUSU UJAUZITO WAKE, KUMBE NI YA STAA HUYUU


Mwigizaji Kajala Masanja amekiri kuwa ni mjamzito huku taarifa zikidai kuwa huenda mhusika wa kiumbe alichonacho ni staa nambari moja wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Risasi Mchanganyiko limeichimba habari kamili.
IMG_4198Mwigizaji Kajala Masanja.


Hivi karibuni, gazeti ndugu na hili la Risasi Jumamosi ndilo lilikuwa gazeti la kwanza kuripoti habari za madai kuwa Kajala ana ujauzito wa kigogo mmoja serikalini (jina tunalihifadhi) lakini mashosti wa karibu wa Kajala wameibuka na kudai kuna asilimia nyingi mimba aliyonayo ni ya Diamond na si kigogo huyo.

ymCTBkp3-1024x1024ymCTBkp3-1024x1024
Staa nambari moja wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
TUJIUNGE NA SHOSTI WA KAJALA
Akizungumza kwa sharti la kuomba hifadhi ya jina, rafiki mmoja wa Kajala alisema ana imani mimba hiyo itakuwa ni ya Diamond kwani kuna kipindi shosti yake huyo aliwahi kuanguka dhambini na staa huyo wa Bongo Fleva.“K (Kajala) kweli alikuwa na yule kigogo (anamtaja jina) lakini sasa waligombana.

DIAMOND ALIPITA?
“Wakiwa wamegombana, Diamond naye alipita si unajua tena zile za kumalizana leo leo tu, sasa nikijaribu kufanya mahesabu tangu Kajala aniambie ana mimba na tangu wagombane na kigogo, naona kabisa Diamond ndiye mwenye asilimia nyingi kuwa baba kijacho,” alisema rafiki huyo.

DIAMOND ANASEMAJE?
Gazeti hili lilifanya jitihada za kumtafuta Diamond ili aweze kuzungumzia kuhusishwa kwake na mimba hiyo, lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi, hakujibu.

TIMU WEMA WASHANGAA
Baadhi ya mashabiki wa Wema ambao walipenyezewa habari ya Diamond kutajwa kuwa mhusika, walimshangaa mwigizaji huyo kwani anazidi kujijengea sifa mbaya.
“Mh! Inashangaza kwa kweli kama ni kweli. Kajala huyohuyo si ndiyo alimuibia Wema yule CK sasa tena ambebee mimba Diamond ambaye alikuwa mpenzi wa Wema!” alisema mmoja wa mashabiki wa Wema.

KAJALA SASA
Gazeti hili lilifunga safari hadi kwa muigizaji huyo na kutaka kujua ukweli wake. Awali, mwanahabari wetu alitaka kujua kama ni kweli Kajala ni mjamzito, akafunguka:
“Ni kweli mimi ni mjamzito na tena ujauzito huu unanisumbua sana, si unajua tena mimi ni mwanamke na ninamshukuru Mungu kwa kunijaalia zawadi hiyo.”

NI MZIGO WA NANI?
Kuhusu mhusika hasa wa ujauzito huo, Kajala hakutaka kuweka wazi, badala yake alisema kila kitu kitakuwa wazi baada ya kiumbe kuzaliwa, wakati wowote mwaka huu.
“Subiri mtoto azaliwe mbona una presha sana? Kila kitu kitakuwa wazi mwaka huuhuu tu, kuwa mpole.”

Kwa nyakati tofauti, Kajala ametajwa kuhusishwa na wanaume kadhaa, akiwemo kigogo huyo wa serikali ambaye hata hivyo, alipoulizwa kama ndiye mhusika halali, alishindwa kukubali au kukataa, ingawa ‘data’ zinaonyesha kuwa wakati akinasa ujauzito huo, alikuwa katika mzozo mkubwa na kigogo huyo.
“Hamna kitu kama hicho, huyo mtu anatapatapa tu, mimi nilifanya naye (Kajala) tu shughuli za kikazi zilipoisha, kila mtu anaendelea na maisha yake, halafu hawa wasanii ni watu wa kuwa nao makini, wana mambo ya kuzusha na kuzushiana mambo ya ajabu kiasi ambacho wanaweza kukosa mambo mengi ya kikazi,” alisema kigogo huyo.

No comments:

Post a Comment