Translate

Thursday, January 7, 2016

NAY WA MITEGO AJISALIMISHA TRA

Mbongo Fleva Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’.


KUFUATIA kasi ya utumbuaji majipu wa Rais DK. John Pombe Magufuli kuendelea kutia hofu kwa wenye mali, Mbongo Fleva Emmanuel Eribaliki ‘Nay wa Mitego’, juzikati alijikuta akijisalimisha kwa kuanika baadhi ya mali zake halali, hasa magari na kuwaita maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kumkagua muda wowote.

NYUMBANI KWAKE Nay aliyasema hayo Januari 4, mwaka huu nyumbani kwake Kimara ya Korogwe jijini Dar mara baada ya kupigiwa patroo na paparazi wetu akimtaka kuweka wazi mali zake baada ya kumtilia shaka kwamba kuna tetesi magari yake hajayalipia kodi.

HAWEZI KUTUMBULIWA Akizungumza kwa kujiamini, Nay alisema katika mali anazomiliki hana wasiwasi wa aina yoyote juu ya kodi ya TRA hivyo kasi ya utumbuaji majipu hata ikianza kupita nyumba moja baada ya nyingine yeye atakuwa msafi namba moja kwani hana gari lenye deni wala kukwepa kulipa kodi.

ATAJA NYUMBA “Kweli kasi ya Dk. Magufuli inatisha, lakini kwangu sina shaka kabisa kwani kila kitu kipo kihalali hivyo hata kama rais atakuja leo kukagua, ataishia kunipongeza kwa kujali kwangu katika kuipatia serikali mapato. “Nina nyumba tatu, moja ina thamani ya shilingi milioni 250, ipo Tabata Kimanga, Dar.

Nyumba nyingine hii ninayoishi, niliinunua kwa shilingi milioni 80. Ukijumlisha na gharama za ukarabati inaweza kufikia milioni mia na kitu hivi. “Nyumba nyingine ipo Kimara Stop Over.
Hii niliinunua kwa shilingi milioni 40 tu. Bado sijaiendeleza,” alisema Nay. ATAJA MAGARI Mbali na nyumba, Nay alisema: “Namiliki magari zaidi ya manne. Toyota Hiace lenye thamani ya shilingi milioni 30, Toyota Port milioni 8, Toyota Land Cruiser Prado ya shilingi milioni 75. Ninajiandaa kuanza kutesa na Range Rover Vogue ambalo tayari nimeshateketeza zaidi ya milioni 180 kwa ajili ya kulinunua.

Mimi nawaita TRA waje, najisalimisha mwenyewe. Siyo mpaka kusakwa.” AMTAJA MASANJA, WEMA Nyota huyo alisema ameamua kujianika kwa vile ameshasoma kwenye Magazeti Pendwa ya Global Publishers yakionesha, TRA wanamsaka mwimba Injili, mchekeshaji na mchungaji Emmanuel Mgaya ‘Masanja’ kuhusu magari yake.

No comments:

Post a Comment