Mmoja kati ya mameneja wa Diamond Platnumz, Sallam amesema kuwa msanii wake yupo booked kuanzia mwezi February mpaka mwezi May mwaka huu.
Akizungumza na Swahili Talk Radio ya nchini Denmark, Sallam alisema yeye na mameneja wenzake wamehakikisha msanii wao anapata show za kutosha.
“Kila mwaka unapoanza lazima tuwe na ajenda ya kutengeneza program ya mwaka mzima, ndio maana mpaka sasa unakuta show zinaanza February na tupo booked mpaka mwezi May,” alisema.
“Kama mimi sasa hivi nipo Ulaya nafanya maandalizi ya tour yetu ya Ulaya na mambo yanaenda poa. Kwa sababu watu wengi walikuwa wanahofu asije akatangazwa anakuja halafu asije ndio maana mimi nipo huku kuweka mambo sawa,” aliongeza.
No comments:
Post a Comment