Translate

Tuesday, March 15, 2016

HII NDIYO KAULI YA MAKONDA BAADA YA KUTEULIWA KUWA MKUU WA MKOA

Headline zilizoongoza kwenye magazeti ya Tanzania March 14 2016 ni kuhusu uteuzi wa wakuu wa mikoa nchini, miongoni mwa waliozikamata zaidi headline hizo ni aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.
Sasa baada ya hayo yote, Paul Makonda akatangazwa kwamba ndio Mkuu mpya wa Mkoa wa Dar es salaam, wakati akitangazwa hakuwa akijua kwamba atatangazwa kuwa Mkuu wa Mkoa.
‘Leo nilikuwa natimiza mwaka mmoja tangu kuteuliwa kwangu kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, pia nilienda kuzindua na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa jengo laupasuaji katika hospitali ya Mwananyamala‘
Alizipata vipi taarifa za kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa? ‘Sina uhakika zaidi kwasababu mtu hata akipiga simu mimi nilikuwa najua ni utani, lakini nilikuja kuamini baada ya kuliona jina langu kwenye karatasi yenye nembo ya Serikali ‘ ;-Paul Makonda

No comments:

Post a Comment