Mgodi wa Dhahabu wa Geita umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa katika utoaji wa fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka Mgodi ambapo kwa Sasa inatekeleza miradi mipya mitatu ambayo ni uchomeleaji,kilimo na ushonaji.
Kwa leo utaona picha mbalimbali za mafunzo ya uchomeleaji wanayopewa baadhi ya vijana ambapo watakapofuzu mafunzo watakuwa na jukumu la kuwafundisha vijana wenzao na hii ni njia ya kuweza kuwainua wakazi wa Geita na kuona fursa za kiuchumi.
Mafunzo yanatolewa bure na hapo chini ni picha mbalimbali za vijana wakipata mafunzo ya uchomeleaji
Huu ni mradi wa kwanza tumeuona usikose kuangalia miradi mingine yenye tija inayofadhiliwa na Mgodi wa GGM wakishirikiana na Serikali
No comments:
Post a Comment