Translate

Friday, April 22, 2016

BALOZI SEFUE AFUNGUKA KUONDOLEWA IKULU


  • KWA kawaida marais wakishaingia madarakani wanakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi waliyemkuta kwa kipindi cha mpito, lakini baadaye wanakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi wakwao, kwa hiyo siyo jambo la ajabu kwangu....
KWA mara ya kwanza aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, amezungumzia kutumbuliwa kwake kulikofanywa na Rais Dk. John Magufuli, kuwa ni kawaida kihistoria na haoni ajabu juu ya h


Balozi Sefue aliyasema hayo wakati akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam juzi baada ya kumalizika kwa hafla ya kuwatunuku vyeti vya shukrani wadau mbalimbali wa Uchaguzi Mkuu mwaka 2015, akiwamo Balozi Sefue, vilivyotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec).

Nipashe ilitaka kujua kwa undani kilichochangia kuondolewa kwake katika wadhifa huo aliodumu nao kwa siku 65 baada ya Dk. Magufuli kuingia Ikulu.
“Kama unajua ilivyo kwenye historia, kwa kawaida marais wakishaingia madarakani, wanakuwa na Katibu Mkuu Viongozi waliowakuta kwa kipindi cha mpito, lakini baadaye wanakuwa na Katibu Mkuu Kiongozi wa kwao, kwa hiyo siyo jambo la ajabu kwangu,” alisema.

No comments:

Post a Comment