Waheshimiwa nawasalimu kutoka Kibondo.
Nina habari zisizokuwa njema. Dada yangu na aliyekuwa Mbunge wetu wa Viti Maalu m Mh. Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya Aga Khan Dar.
Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa cancer tangu mwaka jana.
Kwa sasa niko nje ya Dar na ndio kwanza taarifa hizi zimenifikia, sina taarifa zaidi juu ya mipango ya mazishi, etc. Tutawataarifu baada ya familia kuwa tumeshauriana.
Tundu Lissu.
No comments:
Post a Comment