Translate

Tuesday, May 17, 2016

BREAKING NEWS ... DAVID KAFULILA ABWAGWA TENA UBUNGE

Kafulila apigwa chini 

David Kafulila

KESI YA UCHAGUZI: Mbunge Kigoma Kusini Hasna Mwilima (CCM) ashinda kesi yauchaguzi iliyofunguliwa na David Kafulila (NCCR-Mageuzi - Pichani) Korti Kuu Kanda ya Tabora.
Aliekuwa mbunge wa Kigoma kusini, David Kafulila ameshindwa kwenye kesi yake iliyokuwa ikisikilizwa mahakama kuu kanda ya Tabora kuhusu kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa CCM, Hasna Mwilima.
Kesi hii ilifunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Tabora na kuwa chini ya Jaji Ferdinand Wambari.
Katika kesi hio upande wa mlalamikaji (Kafulila) uliongozwa na mawakili Prof. Abdallah Safari, Tundu Lissu na Daniel Lumenyera, Ili hali upande wa mlalamikiwa (Husna) uliongozwa na wakili Kenedy Fungamtama pamoja na mawakili wa serikali upande wa mwanasheria mkuu.

No comments:

Post a Comment