Watu saba wa familia moja katika kitongoji cha Nyigumba kijiji cha Sima wilaya ya Sengerema mkoa wa Mwanza, wameuawa kwa kukatwakatwa mapanga usiku wa kuamkia leo.
Tukio hilo lililoacha simanzi katika kitongoji hicho, limehusisha ndugu watano wa tumbo moja wakiwamo wanafunzi watatu, waliovamiwa usiku wa manane na watu wasiojulikana na kuanza kukatwa mapanga.
Hata hivyo, mauaji hayo yameibua utata mkubwa kwa tukio na mazingira hayo yaliyoibua utata na simanzi kubwa, lakini chanzo chake bado hakijafahamika.
Wakizungumza na Channel Ten katika kwa nyakati tofauti, baadhi ya wanafamilia wamedai usiku wa saa 8, watu wawili waliokuwa na mapanga walikwenda katika nyumba ya wanafamilia hao na kuanza kuwashambulia, huku wakianza na marehemu Donald ambaye alipambana na wauaji hao, lakini alizidiwa nguvu kabla ya kuangushwa chini na kummaliza.
Inadaiwa kuwa mama wa familia ambaye naye ameuawa katika tukio hilo, alijaribu kufungua mlango wa chumba walicholala wajukuu na watoto wake, lakini njia hiyo aliyowapa mwanya wauaji kuingia ndani ya nyumba na kuanza kuwashambulia kwa mapanga.
Akithibitisha kutokea mauaji hayo katika eneo la tukio, Afisa Mtendaji wa Kata ya Sima, Tamali Lukonge na diwani wa kata hiyo, Lugata Makoye, alimewataja waliouawa kuwa ni mama mwenye nyumba, Augenia Kiwitega, Maria Philipo na Leonard Thomas, ambaye anasoma kidato cha nne Shule ya Sekondari Sima.
Wengine waliouwawa ni Leornad Aloys (darasa la saba) na Mkiwa Philipo mwanafunzi wa darasa la tano wote wa Shule ya Msingi Ijinga, na wengine walifahamika kwa jina moja moja, Samson na Donald kutoka wilayani Ngara mkoa wa Kagera waliokuwa wakulima wa familia hiyo.
Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza kupitia kwa kamanda wake Ahamed Msangi limethibitisha kutokea kwa tukio hilo pamoja na viongozi wengine wa kiserikali akiwemo mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongela wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
No comments:
Post a Comment