Zanzibar. Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amedai kuna vikwazo vya kuwadhoofisha wafuasi wao kushinikiza kudai ushindi walioupata kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka jana.
Maalim Seif alizitaja mbinu hizo ambazo hakutaja zinafanywa na nani kuwa ni vikwazo na visingizio vinavyoandaliwa kuwarejesha nyuma wanachama hao kutekeleza azma ya kudai ushindi ambavyo ni pamoja na kuteswa na kubambikiwa kesi, lakini hayo yote si lolote wala chochote.
Kiongozi huyo alisema hayo katika mkutano huo uliolenga kufanya majumuisho ya ziara aliyoianza Mei 13, mwaka huu katika wilaya za Unguja na Pemba.
No comments:
Post a Comment