Bado headlines za mshambuliaji wa kimataifa wa Senegal anayeichezea klabu yaShanghai Shenhua ya China Demba Ba zinaendelea kuchukua nafasi, Demba Baambaye ana umri wa miaka 31 alitarajiwa na wengi huenda akatangaza kustaafu soka mapema kutokana na kuvunjika mguu wake wa kushoto.
Ba amenukuliwa na radio ya China ya Monte Carlo akiwa hospitali kuwa hatazamii kustaafu karibuni kutokana na kuvunjika sehemu mbaya ya mguu wake wa kushoto, pamoja na hayo Demba Ba amesema hajafanyiwa upasuaji kamili kutokana na yeye mwenyewe kutaka kwenda Ulaya kutibiwa.
“Sikuwa nimewaruhusu wanifanyie upasuaji kamili kwa sababu nilitaka kwenda Ulaya kutibiwa lakini kutokana na hali yangu haiwezekani hivyo doctor atakuja hapa akitokea Ulaya, kiukweli sina mpango wa kustaafu mapema kwa sababu ya majeruhi yangu, kwani nimeona Hatem Ben Arfa akipata majeraha kama haya na amerudi kucheza soka”
“Jeraha langu la mguu ni sawa tu na Hatem Ben Arfa, hivyo kwa sasa kinachohitajika ni mimi kupata huduma iliyobora ili niweze kurudi uwanjani haraka, msimu wa Ligi China unamalizika November na msimu mpya utaanza March, hivyo nitajitahidi kuhakikisha narudi mapema uwanjani kabla ya kuanza kwa msimu ujao”
No comments:
Post a Comment