ATCL YAANZA KUFUFUKA
Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imetangaza ajira mpya 28 lengo likiwa ni kuifufua kampuni hiyo.Nafasi hizo zilizotangazwa na ATCL ni marubani wanne, wahandisi sita na wahudumu 18.
Mei 12 mwaka huu, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akiwa kwenye mkutano wa tatu wa Bunge la Bajeti, alisema Serikali imekusudia kuagiza ndege mbili ili kuhakikisha ATCL inainuka katika huduma za usafiri wa anga.Mbarawa alisema: “ATCL ina wafanyakazi 200, tutaajiri upya wafanyakazi na watakaokuwapo ni wale watakaoendana na idadi ya ndege, hatutaki kuwa na wafanyakazi wanaopiga maneno, lengo letu ni kuifufua ATCL.”
No comments:
Post a Comment