Translate

Tuesday, August 23, 2016

HII NDIYO DAWA YA KUZUIA MAANDAMANO YA VYAMA VYA SIASA

JAJI MUTUNGI (2)




Kufuatia sintofahamu inayoendelea kuhusu vyama vikuu vya Siasa, na kuzua hofu kwa wananchi baada ya vyama hivyo kutangaza kufanya maandamano ,jambo ambalo msajili amelitolea ufafanuzi.

Ambapo Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini Jaji Fransis Mutungi amevitaka vyama vya Siasa nchini vyenye mpango wa kufanya maandamano au mikutano ya kuhamasisha wanachama wake, viache ili kutafuta suluhu za changamoto zinazowakabili kupitia majadiliano ya pamoja.
Jaji Mutungi ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na Waandishi wa habari ambapo amesema migogoro na changamoto za kisiasa zinazo vikabili vyama vya siasa zisipojadiliwa vizuri katika meza moja ya majadiliano baina ya pande mbili,inaweza kusababisha kuvunjika kwa amani ambayo imejengwa kwa muda mrefu na waasisi wa Taifa hili.

Jaji Mutungi amesema akiwa kama Mlezi wa Vyama vya Siasa na Katibu wa Baraza la Vyama vya Siasa nchini amevitaka Vyama vya Siasa kutumia Mkutano Maalumu wa Baraza la Vyama vya Siasa unaotarajia kufanyika Agosti 29 na 30 mwaka huu kujadili changamoto zinazowakabili kwa njia ya amani na maridhiano badala ya kufanya maandamano ambayo yanaweza kuhatarisha amani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment