Harmonize
Andrew CarlosMASTAA wa Bongo bwana! Baada ya kukopi na kupesti staili ya kuimba na biti zao nyingi kufanana na za Sauz na Nigeria ni kama wamehamia kwenye staili mpya ya usukwaji nywele inayotumika hasa kwa mastaa nchini Marekani.
Ukiwaangalia muonekano wa vichwa vyao, baadhi ya mastaa hawa wakiongozwa na Jux, Romy Jones, Harmonize na wengine kibao utagundua kuna kitu wamekopi na kupesti kutoka kwa mastaa wa mbele ambao ni Chris Brown, Post Malone, The Game, Omario na wengineo
Inaitwaje?
Staili hii iliyotokea kujizolea umaarufu mkubwa kwa mastaa mbalimbali hususan wa muziki inajulikana kama Dutch Braid japokuwa chimbuko hasa la staili hii lilikuwa likijulikana kama French Braid.
Omarion
Staili hii ipoje?Usukwaji wake huwa wa nywele kuanzia njia mbili kubwa kisha kwa nyuma inafungwa ama kuachiwa mikia.
Mastaa wengi wa kike kama Kim Kardashian, Karrueche na wengineo wanapenda kusuka njia mbili ndefu za kuacha mkia ukining’inia na kwa upande wa mastaa wa kiume, pande zote za pembeni hunyoa na katikati husuka njia mbili ama tatu kisha huzifunga kwa nyuma.
Post Malone
Ukicheki baadhi ya video zake za hivi karibuni alizofanya na wakali kama Young Thug, 50 Cent na Kanye West kichwani kwake utamuona katika muonekano wa Ki-dutch.
The Game
Rapa huyu kutoka Los Angeles, Marekani aliiweka picha mtandaoni akiwa saluni katika matengenezo ya staili ya Dutch na baada ya hapo alipewa shavu la kutosha kutoka kwa mashabiki.
Chris Brown
Chris ambaye ni baba wa mtoto mmoja, Royalty amekuwa akitupia picha zake mitandaoni zikimuonesha katika muonekano wa Ki-dutch lakini kwa staili mbalimbali.
Jux
Jux ameonekana kula sahani moja na Chris Brown. Mara ya kwanza Chris alitengeneza staili hii ya Dutch kizamani kwa kuning’iniza nywele mbili mbele na nyuma kubana, Jux alipoona akakopi na kupesti.
Chris akabadili staili hiyo na kunyoa za pembeni, nyuma akizibana. Jux kuona hivyo naye akaiga tena ambayo ndiyo anayo hadi sasa.
Harmonize
Staa huyu anayebamba na Ngoma ya Matatizo, baada ya kuongeza michoro kadhaa mwilini mwake (tattoo), ameamua kubadili na staili ya nywele.
Alichokifanya kichwani kwake, amejaribu naye kukopi na kupesti staili ya Dutch ambapo kwa sasa amekuwa akitupia picha nyingi na vipande vya video akiinamisha kichwa ili mashabiki wake waione staili hiyo mpya ya nywele.
Romy Jones
Hivi karibuni, binamu na DJ wa staa wa muziki wa Bongo Fleva, Diamond, Romy Jones katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Next Door, jijini Dar aliingia na sapraizi kichwani kwake akiwa katika muonekano wa Ki-dutch.
Kama ulivyo muonekano wa nywele kwa sasa wa Omario, Chris Brown na The Game kwa Rommy hakuna tofauti yoyote kwani naye amekopi na kupesti tu.
No comments:
Post a Comment