Translate

Sunday, October 16, 2016

NDEGE MPYA YAENDA KIGOMA NA KURUDI BILA ABILIA!

NDEGE mpya ya Bombardier Dash 8- Q400, iliyonunuliwa hivi karibuni imetua kwenye Uwanja wa Ndege wa Kigoma ikiwa ni ukaguzi na majaribio ya mwisho kabla haijaanza kubeba abiria. Ndege hiyo ni kati ya mbili zilizonunuliwa na serikali na kukodishwa ATCL.Akizungumza muda mfupi baada ya kutua uwanjani hapo jana Mhandisi wa Ndege wa ATCL, John Chaggu amesema baada ya safari hiyo ndege hiyo itakuwa tayari kubeba abiria.Amesema, katika majaribio hayo alikuwa na wakaguzi wawili wa ndege kutoka Canada wa kampuni iliyotengeneza ndege hiyo.Chaggu amesema, safari yao kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma iliwachukua saa mbili angani.Ilitua Kigoma saa 11:00 jioni na kuondoka saa 12:18 jioni .Ndege hiyo ilitarajiwa kuendelea na safari ya ukaguzi kwa kwenda kutua Uwanja wa Ndege wa Mwanza na baadaye kurudi Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment