
Weekend hii katika mitandao ya kijamii kumesambaa video inayomuonyesha malkia wa filamu nchini Wema Sepetu akiliwa denda na model Calisah, imeweza kumsababishia Calisah matatizo.
Calisah amesema hayo alipokuwa akizungumza na Bongo5 juma tatu hii amedai kuwa video hiyo imemsababishia matatizo katika familia yake pamoja na kumpoteza bibi yake kwa presha
Calisah amesema hajui ni nani ambaye amesambaza video hiyo mtandaoni kwani walikuwa nayo yeye pamoja na Wema.
“Nilikuwa nachati na Wema kawaida ghafla nikaona notification, kufungua ndio nikakuta hiyo video na mimi ndio nilikuwa mtu wa kwanza kumuuliza Wema kwa sababu video nilikuwa nayo mimi na Wema,” alisema Calisah.
No comments:
Post a Comment