Moja kati ya taarifa ambazo zilichukua headlines June 21 2017 ni taarifa kutoka Club ya Yanga ambapo Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa alitangaza na kuweka wazi kuwa Haruna Niyonzima ambaye mkataba wake na Yanga unamalizika July, Na wameshindwa kufikia makubaliano ya kumuongezea mkataba mpya.
Stori zilizoko kwa sasa kwenye mitandao ya kijamii ni kuwaa Haruna Niyonzima anatarajia kujiunga na Club ya Simba na moja kati ya Mashabiki wakubwa wa Club hiyo mkali kutoka Bongoflevani Mwana FA ametumia mtandao wake wa Twitter na Instagram kuyaandika maneno kwenye picha ya Haruna Niyonzima
‘Haruna mwenyewe ndio hufanya mambo haya???aaaah,sitaki mimi .ama kweli akupigae ngumi ya jicho,na we mpige ya sikio akikuuliza unaonaje na we muulize.’Mwana FA
No comments:
Post a Comment