Translate

Friday, June 9, 2017

KIBITI:- WATU WAWILI WAMEPIGWA RISASI NA WAHALIFUA KUTOKOMEA NAO KUSIKOJULIKANA



PWANI: Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Onesmo Lyanga amesema kuwa, watu wawili wamepigwa risasi katika Kijiji cha Nyamisati, Kibiti, kisha waliofanya uhalifu huo kuwachukua majeruhi na kuondoka nao kusikojulikana.

Awali taarifa zilizotolewa na mashuhuda wakazi wa kijiji hicho zilisema watu watatu wameuawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia leo ambao walitajwa kuwa ni Hamid Kidevu,Yahaya Makame na Moshi Machela.
Mkuu wa wilaya ya Kibiti Gullamuhusein Kifu alisema ameliagiza Jeshi la Polisi wilayani humo kwenda eneo hilo kwa ajili ya uthibitisho.
Lakini akizungumzia tukio hilo leo asubuhi, Kamanda Lyanga amesema watu wawili wamejeruhiwa kwa risasi na wahalifu kutokomea nao kusikojulikana.
“Tunaendelea na uchunguzi.” Amesema Kamanda Lyanga.

No comments:

Post a Comment