Translate

Friday, August 4, 2017

BREAKING NEWS :- MAHAKAMA KUU YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA WABUNGE WALIOFUKUZWA CUF


Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017 imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa  Viti Maalumu waliofutwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba ya kutaka wabunge wateule 8 wasiapishwe na Bunge.

Uamuzi huo, umetolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambaye amesema ametupilia mbali pingamizi hilo la zuio la kuapishwa kwa Wabunge hao 8 na kwa mantiki hiyo, Wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao wanaweza kuapishwa.

No comments:

Post a Comment