Serikali ya Korea Kaskazini imesema kuwa imepata taarifa kutoka wizara ya ya mambo ya ndani yaKorea Kusini kuwa mawakala wa kundi la kigaidi linaloungwa mkono na Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA) na shirika la ujasusi la Korea Kusini wameingia nchini humo kwa lengo la kumuua rais wa nchi hiyo.
Korea Kaskazini imesema kuwa kabla ya kutekelezwa kwa azmio hilo itahakikisha inawasaka mawakala hao na kuwaangamiza bila huruma
Imeyasema hayo wakati wasiwasi ukiongezeka kati ya Marekani na Korea Kaskazini dhidi ya tuhuma za matumizi ya silaha za nyuklia.
Aidha, shirika la habari la Korea Kaskazini limesema kuwa njama hiyo inahusisha kutumiwa kwa silaha kali ya bio-kemikali pamoja na kemikali yenye miale ya sumu.
Hata hivyo, mwishoni mwa wiki, Rais Marekani Donald Trump alisema anatamani kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un, ili waweze kufanya mazungumzo.
No comments:
Post a Comment