Translate

Sunday, November 5, 2017

UJUMBE WA MH TUNDU LISSU KWA WAPIGA KURA.




Mbunge Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu ametuma ujumbe kwa wapiga kura kwenye kata zenye uchaguzi ya kwamba kuwapatia kura za ushindi Chama Cha Mapinduzi ni kufurahia na kuruhusu mateso.
Ujumbe huo kutoka kwa Lissu kwenda kwa wapiga kura umefikishwa na Diwani wa Sombetini  Arusha, Ally Bananga ambaye amefika hospitali ya Nairobi nchini Kenya anakopatiwa matibabu mbunge huyo.Kupitia ukurasa wake wa Instagram Bananga ameandika, "Nendeni mkawaambie watu kwenye kata zenye uchaguzi kuipa kura ccm ni kufurahia na kuruhusu mateso yetu yaendelee!!...."  Ujumbe alioutoa Lissu kupitia diwani BanangaAmeongeza kwamba 'Hawa watesi wetu wako katika hatua za mwisho, kama wanajiamini kwa nn wanawawekea mizengwe wagombea wetu ili wao wapite bila kupingwa"

No comments:

Post a Comment