Translate

Tuesday, December 19, 2017

CHADEMA YAKANUSHA KUCHUKUA FOMU YA UBUNGE SINGIDA KASKAZINI



Mkurugenzi wa idara ya habar na mawasiliano Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Tumain Makene amezikana taarifa za kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika uchaguzi wa marudio Jimbo la Singida Kaskazini mkoani Singida.

Chama cha demokrasia na maendeleo kupitia mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) ameongea na chombo flani cha habari jijini DAR ES SALAAM juu ya kuchukua fomu za kugombea ubunge jimbo la singida kaskazini.
Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya uchaguzi amesikika akiongea asubuhi hii wakati akiojiwa na Radio Clous fm,akisema kuwa Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA imekanusha habari ya kuchukua formu ya kugombea UBUNGE katika uchaguzi wa marudio Jimbo la Singida kaskazini,Mkoani singida.
chama hicho cha demokrasia na maendeleo CHADEMA hakijateua mgombea kuwania nafasi nafasi ya ubungekatika uchaguzi huo wa marudio,jimbo la singida kaskazini.

Mapema leo kupitia kipindi cha Break fast cha Clouds fm, Tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kupitia Mkurugenzi wake Bw Ramadhani Kailima amesikika akisema kuwa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wamechukua fomu ya kugombea uchaguzi huo wa marudio unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Tumaini makene amesema kuwa Chadema wanapenda vyombo vya habari na jamii kwa ujumla wajue kuwa Chadema hawajateua mgombea yoyote kuchukua fomu ya kuwania nafasi ya ubunge katika uchaguzi wa marudio jimboni humo.
Aidha Makene amemtaka Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Ndugu Ramandhani Kailima atambue kuwa yeye hana mamlaka wala hawezi kuwa msemaji kwa hatua ya sasa kwani suala la kugombea ubunge ndani ya Chadema linasimamiwa na Kamati kuu ya Chama.
“Tunafuatilia kupata taarifa za kina kuhusu msingi wa wa kauli hiyo ya Mkurugenzi, kisha tutatoa taarifa kamili katika hatua ya baadae”. Amesema Mkurugenzi wa idara ya habari na mawasiliano Chadema Tumaini Makene.
PICHA:TAARIFA KUHUSU KUGOMBEA UBUNGE SINGIDA KASKAZINI

No comments:

Post a Comment