Hii ni Mara ya pili kwa ndugu Kalumuna kutangaza kukihama Chama cha ACT Wazalendo ambapo mara ya kwanza alitangaza kufanya hivyo kwenye kampeni za CCM katika Jimbo la Kinondoni.
Hata hivyo Chama cha ACT Wazalendo kupitia kwa Afisa Habari wake Abdallah Khamis alieleza kuwa Chama hicho kilishamuondoa kwenye ukatibu wa Mkoa na Kamati Kuu miezi mingi nyuma.
Mmoja wa watu waliotajwa Kwenye orodha ya leo iliyosomwa na Kalumuna, Robert Kihiri ambaye alitajwa Kama Mwenyekiti wa Vijana wa Jimbo la Ubungo amesema “Wapuuzeni hao watu, ni wahuni. Wamenifuatilia mimi kwa simu hadi kwangu wamefika kunishawishi nijiunge CCM, nimekataa. Mimi bado ni mwanachama wa ACT Wazalendo na sina Shaka na mwenendo wa Chama chetu. Sijakihama Kama wanavyodai,” amesema Robert Kihiri.
No comments:
Post a Comment