Translate

Monday, March 12, 2018

YANGA YATOA KIPIGO KWA STAND UNITED, WAIFIKIA SIMBA KILELENI


Mabingwa wa kihistoria wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Dar es Salaam Young Africans imefanikiwa kupata pointi tatu muhimi dhidi ya timu ya Stand United baada ya kuchomoza na ushindi wa mabao 3 – 1 mchezo uliyopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


Mabao ya mabingwa hao watetezi yamefungwa na Mhilu na Ajibu katika kipindi cha kwanza na Obrey Chirwa akihitimisha mabao matatu kipindi cha pili huku kwa upande wa Stand United likifungwa na Vitalis Mayanga.

Kwa matokeo hayo unaifanya Yanga SC kuwa na jumla ya alama 46 sawa na vinara Simba SC wakiwa na tofauti ya magoli ya kufungwa na kufunga.

No comments:

Post a Comment