Translate

Tuesday, September 8, 2015

MAGUFULI AISAMBALATISHA UKAWA MOROGORO!

 VIDEO: Uongozi wa CHADEMA Kilosa (M/kiti, Katibu), wahamia CCM muda huu
Viongozi wakuu wa Chadema wilaya ya Kilosa na baadhi ya wanachama wametangaza kujiunga rasmi na CCM baada ya kuchoshwa na siasa za Chadema ambazo wameona hazina haki.
Viongozi hao waliohamia CCM ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Kilosa Ndugu Selemani Simba, Katibu wa Chadema wilaya hiyo Ndugu Ibrahim Abdallah Selemani, aliyekuwa Katibu wa Jimbo la Kilosa Mussa Ngongo na aliyejitambulisha kama mwanachama kiherehere wa Chadema Bi.Oliver Mollel.
Viongozi hao walitangaza kukihama chama cha Chadema kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM mbele ya mgombea wa urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Kilosa town uliofanyia jana!

No comments:

Post a Comment