Huku hari ya Ukawa ikizidi kuwa mbaya Jimbo la Geita mjini baadhi ya makada wa Chadema akiwepo na Deo Shinyanga wametumia jukwaa la mgombea udiwani kata ya Kalangalala kuionya tume ya uchaguzi na jeshi la polisi kutenda haki tarehe 25 October
Wakati akihutubia Ndugu Deo Shinyanga. huku akiwanukuu baadhi ya wapigania uhuru na haki duniani Martine Luther King Jr na Nelson Madiba Mandela alisema mda wa watanzania kupata uhuru wa haki umewadia na kuwaomba watanzania kukipa ridhaa Chadema ili kiwaletee maendeleo
Huku Deo Shinyanga akitoa maneno hayo yaliyokonga nyoyo ya wapenda mabadiliko baadhi ya makada wa chadema walitumia lugha kali na za vitisho ili kuwatia hamasa hasa vijana ili kujiaandaa kilinda kura kwa gharama yoyote ile .Huku wakiwaomba vijana kuandaa mawe ili kukabiliana na polisi iwapo watapokonya haki yao kwa nguvu
No comments:
Post a Comment