Naftar Mlawa ‘Nuh Mziwanda’
Zikiwa zimepita siku chache tangu wasanii waliokuwa wapenzi, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na Naftar Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kuachana, imedaiwa kuwa mwanaume huyo amefulia na kujikuta akila kwa mama lishe huku akidaiwa kodi ya chumba anachoishi.
Zuwena Mohamed ‘Shilole’
Chanzo makini kimeiambia Showbiz Xtra kuwa wawili hao wakati wakiwa katika uhusiano wa kimapenzi, Shilole ndiye aliyemlipia kodi ya chumba ambacho Nuh anaishi mpaka sasa kilichopo maeneo ya Sinza-Kwa Remmy hivyo muda ukiisha kuna uwezekano akatolewa vitu vyake nje kwani hawezi kumudu kulipa kodi.
“Yaani sasa hivi Nuh amefulia vibaya kwani anakula kwa mama lishe tofauti na zamani alikuwa haonekani akila hapa mtaani, unajua Shilole ndiye aliyekuwa msaada mkubwa kwake sasa wameachana itakuwa ni shida sana kwake maana ndiye aliyemlipia kodi ya chumba anachoishi,” kilisema chanzo.
Baada kuzinyaka habari hizo paparazi wetu alimtafuta Nuh ambaye alisema kuwa siyo kweli bali Shilole amekuwa akimsema maneno mengi ya uongo
.
“Mdomo ni jadi yake lakini ukweli ni kwamba hiki chumba ninachoishi nimelipa kodi mwenyewe kwa fedha ambazo nilipata kwenye kampeni na sijalipiwa na mtu, wakati tuko wapenzi mara nyingi alikuwa akija kulala hapa.
“Kuhusu kufulia jamani sijafulia nakula kwa mama lishe kwa sababu ndiyo maisha yetu Watanzania, zamani nilikuwa nakula nyumbani ndiyo maana nilikuwa sionekani kwa mama lishe.”
Kwa upande wa Shilole alipoulizwa kuhusiana na madai hayo ya kumpangia chumba alikuwa na haya ya kusema;
“Sitaki kusikia habari za huyo mtu kwa sababu nilishamtoa kwenye mawazo yangu, sina muda wa kumzungumzia huyo mtu kabisa.”
No comments:
Post a Comment