Translate

Friday, February 12, 2016

VITA KALI IMEANZA KATI YA TEAM WEMA NA NEY WA MITEGO


Team Wema wana hasira na Nay wa Mitego baada ya rapper huyo kumchokoza malkia wao kwenye ngoma yake mpya ‘Shika Adabu Yako.’

Kwenye wimbo huo Nay anarap:

Wema Sepetu una mimba kweli, au ndo kiki za msimu?
Miezi tisa sio mingi, isije ikakugharimu
Na siku hazigandi tayari ushakuwa bibi
Na unakoelekea utatafuta kiki hadi kwa Fid

Mistari hiyo hawajaipokea vizuri na sasa Team Wema wako kooni kwa Nay wa Mitego wakilipiza kisasi. Wanazitengeneza picha za rapper huyo na kuzikiweka lipstick na mawig/weaving kumpa muonekano wa mwanamke.

Hata hivyo Nay haoneshi kutishika.

Asanteni wapenda muziki mzuuuriii..!! Haya wale waliopanic twendeeee tililikeniiiiiiii ila adabu mmeshika ndio maana mapovu yanawatokaaaa,” ameandika kwenye post mpya ya Instagram

No comments:

Post a Comment