Translate

Friday, April 28, 2017

JE WAJUA :- MAKOMBORA YA MAREKANI NDIYO BORA ZAIDI DUNIANI



Baada ya vita kuu ya pili ya dunia kuisha,marekani na Soviet Union walianza kushindana namna ya kutengeneza Intercontinental Ballistic Missile yani (ICBM),ni kombora ambalo husafiri angani bara hadi bara lingine.makombora haya hutumia mafuta yanayoungua kwa kiwango cha juu kwa ajili ya kusafirisha kilipuzi.


Hivyo Soviet Union ikaibuka na Scud na Marekani ikaibuka na Minute Man.Baada ya hapo walikuja na aina mbalimbali za makombora lkn hapa tunaongelea MINUTE MAN,

Miaka ya 50 Kampuni la Boeing ndiyo lilitumika kutengeneza kombora hili hivyo kufika mwaka1962 kombora la kwanza lilikamilika ambalo ni:-
     
          1962=Minute Man-1 ,

Kombora hili lilikuwa na uwezo mkubwa lkn kufuatana na tekinolojia ya udakaji wa mabomu wa wakubwa hawa wawili,Marekani ikalazimika kutoa muundo mpya wa Minute Man.Hivyo

          1965=Minute Man-2

Ilizinduliwa ilikuwa na uwezo wa kudanganya rada ya adui na kupenya Mfumo wa ulinzi kufanikisha shambulizi,lkn bado hawakuishia hapo utafiti uliendelea hadi

           1970=Minute Man-3

Huyu ndiyo akawa hatari zaidi angani,anadanganya rada ya adui na kuiunguza system yake isifanye kazi yake na kukimbia kwa speed ya 28.176km/saa yani kilomita 8 inaenda kwa sekunde,kufumba na kufumbua imepita na inapita juu umbali wa kilomita 1,120 kwenda juu tokea chini ardhini na kwenda umbali wa kilomita 13,000.

Lina uzito wa tani 35 na kilo 300,Urefu wake ni Futi 60,linafyatuliwa tokea ardhini na linatumia mafuta,japo ni tofauti na mabomu ya nchi zingine mfano Urusi au korea kaskazini ambayo hutumia muda mwingi kupasha moto mafuta kabla alijalipuliwa kwenda angani kitendo ambacho humpa adui nafasi ya kukishambulia kabla hakijapaa.Hivyo kwa Minute Man ni tofauti kabisa kwani halina muda wa kusubiria kupata moto,lenyewe ukiruhusu tu linaanza kupasua anga na ndiyo maana likaitwa MINUTE MAN.

Kombora hili linabeba Nyuklia au kichwa cha kawaida cha kivita,hivyo marekani ana kikosi kinachoitwa AIR FORCE GLOBAL STRIKE COMMAND,ni kikosi kinachohusika na mashambulizi ya masafa marefu Popote duniani,hivyo ndiyo wamekabidhiwa mabomu haya hatari.hadi sasa hakuna nchi yenye uwezo wa kuzuia shambulizi la kombora hili.







No comments:

Post a Comment