.
Baada ya Raila Odinga kuteuliwa kuwa mgombea wa urais kupitia muungano wa Nasa Uhuru Kenyatta amesema muungano huo wa upinzani hauna nia njema kwa Kenya zaidi ya kugawana vyeo tu,,
Uhuru Kenyatta Amesema viongozi wa upinzani wakiongozwa na Raila Odinga wamekosa malengo zaidi watumia nguvu nyingi kupigania madaraka na kugawana vyeo badala ya kupigania wakenya..
Uhuru Kenyatta amesema viongozi wao walikuwa serikalini kwa muda mrefu sana lakini hawakufanya chochote cha maana..
#Akasema viongozi wao hao siyo watu wanaoheshimu demokrasia nchini zaidi ya kufanya maandamano...
#Kenyattaa akaenda mbali kuwa viongozi wao siyo watu wanaoheshimu katiba akatolea mfano viongozi wao walivyotengeneza nafasi ya waziri mkuu na naibu waziri wakati havikuwepo ndani ya Katiba ya Kenya
Uhuru Kenyatta ametoa kauli hii wakati alipofanya ziara katika maeneo ya akaunti ya Kiambu huku upinzani wakifanya mkutano Nairobi ambapo wameweza kumtaja mkombea wao urais ambaye ni Raila Odinga
No comments:
Post a Comment