Translate

Monday, May 22, 2017

KILICHOMKUTA LOWASSA NDANI YA CCM 2015 NDICHO KITAKACHOMPATA WILLIAM RUTO NDANI YA JUBILEE




#Naomba tuweke kumbukumbu leo kilichomkuta Edward Lowassa mwaka 2015 ndani ya Ccm wakati Kikwete anamaliza muda wake ndicho kitakacho mkuta William Samoei Ruto mwaka 2022 wakati rais Uhuru Kenyatta atakapokuwa anamaliza muda wake kama atachaguliwa tena mwaka huu..
#Niliwahi kusema kuwa inawezekana wa upinzani wasifanikiwe kushinda uchaguzi wa mwaka huu lakini uwezekano upinzani kushinda mwaka 2022 utakuwa mkubwa kwasababu chama cha Jubilee wakati huo kitakumbwa na mpasuko mkubwa sana ,,

#Siku zote wanasiasa siyo wa kuamini sana na kwenye siasa hakuna rafiki w kudumu au adui wa kudumu kwahiyo haitakuwa jambo la ajabu Uhuru Kenyatta kutumpa William Samoei Ruto Baada ya kumtupa ,ebu tazama mifano hii
-Lowassa alifanya kila aina ya msaada ya kumpigania Kikwete kuingia madarakani mwaka 2005 lakini kikwete huyo huyo ndiye aliongoza kikao kizito cha kukata jina la Lowassa Dodoma ili hasigombee urais kupitia Ccm/ 

 -Thomas Sankara alishirikiana na rafiki yake wa damu Blaise Compaoré kufanya mapinduzi mwaka 1983 ambayo yalileta neema kwa wananchi Burkina Faso lakini mwaka 1987 huyo rafiki yake aliongoza mapinduzi ya kumpindua pamoja na kumuua
-Raila Odinga alitembea kila kona ya kenya kumuombea kibaki kura mwaka 2002 lakini kibaki alipoingia madarakani rais amkamtimua Odinga kwenye serikali yake
-Jaramogi Oginga Odinga Alipoitwa na Waingereza kuunda serikali naye awe Waziri Mkuu . Jaramogi aliwaambia hasiingewezekana. “Bila Jomo Kenyatta hakuna Uhuru nchini kenya wakati huo Jomo Kenyatta alikuwa amefungwa jela kwahiyo Jaramogi Odinga waliendelea na mapambano moto unaliendelea kuwaka ili Kenyatta atoke jele huku wakikataa ofa ya uongozi kutoka kwa wakoloni
 Kwa Jaramogi, alitambulika kitaifa, aliheshimiwa na nguvu ya kisiasa,Na hivyo angeweza kuchukua usukani kirahisi kutokana na ofa ambayo alikuwa amepewa na wakoloni . Badala yake alimpigania Jomo kuhakikisha anatoka jela Lakini Jomo alipoingia madarakani na kutamka “Haraaaambee”, mtu wa kwanza kumtimua alikuwa ni aliyemsaidia kuingia madarakani Jaramong Odinga
- Tom Mboya mwanasiasa nchini Kenya aliyekuwa mwerevu mwenye akili kama nguchiro wakati Jomo akiwa
maadaakani alipata maradhi ya tumbo pamoja na msukosuko aliokuwa ndani ya chama cha KANU aliyemsaidia Jomo Kenyatta alikuwa ni Mboya aliyejitokeza na kuuondoa msukosuko hiyo lakini mwaka mmoja au zaidi baadaye alipigwa risasi, kufa na kusahaulika kabisa . \
-Wanasiasa Charles Njonjo. GG Kariuki ndio waliomsaidia sana Daniel Arap Moi kuingia maadarakani lakini alipoongia madarakani akawatupa nje ya serikali haraka
 bila uhuruma.
#Wembe huu ndio utakao tumika kumnyoa William Samoei Ruto mwaka 2022 wakati Uhuru Kenyatta anamaliza muda wake kama atafanikiwa kuchaguliwa tena mwaka huu....
#Zipo taarifa zinasema kuwa Uhuru Kenyatta ana mkataba na familia ya Danile Moi ndio o maana wa chama cha Kanu likuwa kinapanga kuungo mkono upinzani lakini baada ya Mama yake Kenyatta bi, Ngina Kenyatta kwenda kukutana na mzee Moi mara mbili na kufanya vikaoa vya siri huku rais Uhuru Kenyatta alienda kukutana na mzee moi mara moja na kufanya kikao cha siri, Maamuzi ya kanu ya kuunga mkono upinzanni yalibadilika ghafra na kutangaza kumuunga mkono Uhuru Kenyatta,,,,
#Mwenyekiti wa Chama cha kanu ndugu GEDEON MOI ambaye ni mtoto wa Moi ametangaza wazi kumuunga mkono Uhuru Kenyatta lakini hapo hapo akiwa na uhasama wa kiasa na William Samoei Ruto ....Kwa vyovyote mtoto wa Moi ana mpango wa kugombea urais mwaka 2022 baada Uhuru Kenyatta kumaliza muda wake..
SWALI LINAKUJA
Uhuru Kenyatta atamuungani nani mkono wakati tayari ana mikataba ya watu wawili tofauti???
Mkataba wa yeye na familia ya Moi
mkataba wa yeye na William Samoei Ruto


Mwandishi  wa ujumbe huu   Respicius Francis ambaye ni mmiliki wa mtandao wawww.tanzaniaclassic.com.

No comments:

Post a Comment