Juzi ijumaa msafara wa CCM wa kampeni za udiwani kata ya Murieti ulikutana na msafara wa CHADEMA na hivyo kupelekea vurugu. Yani wakati CCM wanafunga mkutano wao maeneo ya "Kwa Mrombo", wakati wanaondoka wakakutana na gari la matangazo la Chadema. Ikumbukwe CCM walikuwa wameshamaliza mkutano maana ilikuwa ni zaidi ya saa 12 jioni.
CCM wakiwa njiani kutoka kwenye mkutano wao, ndipo walipokutana na gari ya matangazo ya Chadema ambapo inadaiwa wafuasi wa CCM walianzisha matusi dhidi ya Chadema na hivyo kusababisha vurugu. Katika vurugu hizo mgombea wa CCM katika kata hiyo Ndg.Francis Mbise anadai kujeruhiwa kwa kupigwa teke (moja) kifuani, hali iliyomfanya alazwe hospitali ya Mt.Meru.
Baada ya vurugu hizo Polisi mkoani humo waliwakamata wafuasi 12 wa Chadema akiwemo Katibu wa CHADEMA Arusha Ndg.Innocent Kisanyage kwa tuhuma za kumshambulia na kumjeruhi mgombea udiwani wa CCM ndugu Mbise.
HARUFU YA HUJUMA:
Mosi; ni kukamatwa kwa wafuasi 12 wa Chadema na kushtakiwa kwa kumshambulia na kumjeruhi Mbise. Lakini maelezo ya Mbise aliyotoa polisi, Hospitali ya Mt.Meru na mbele ya waandishi wa habari anaeleza kuwa alipigwa teke kifuani. Tafsiri ya teke maana yake ni moja. Angepigwa mengi angesema mateke. Msikilize Mbise mwenyewe hapa akieleza kuwa amepigwa teke (moja) kifuani https://www.youtube.com/watch?v=Ia7BqX2BKDM
Sasa kama mlalamikaji anadai kupigwa teke moja inakuaje polisi wakamate watu 12 na kuwafungulia wote mashtaka ya kujeruhi? Wamemjeruhi nani? Watu 12 wanawezaje kumjeruhi mtu kwa teke moja? Ina maana wote 12 walishirikiana kurusha teke moja kwa Mbise? Haya ni maajabu.
Ndio maana siku zote huwa nasema CCM wanapenda namba lakini hawajui hesabu. Kama mlitaka kukamata wafuasi wengi kiasi hicho mngemfundisha huyo mgombea jinsi ya kujieleza. Sasa yeye kasema amepigwa teke moja, halafu mmekamata watu 12. Teke gani linarushwa na watu 12? Anyway, mmekamata na gari pia. Je gari nalo lilirusha teke?
Pili ni mkanganyiko wa taarifa kati ya polisi na maelezo ya mlalamikaji. Jana RPC wa Arusha Charles Mkumbo alilieleza gazeti la Mwananchi kwamba wafuasi hao wa Chadema walimshambulia Mbise na kumjeruhi maeneo mbalimbali ya mwili wake. Yani maelezo ya RPC yanacontradict maelezo ya mlalamikaji mwenyewe. Mbise anasema amepigwa teke moja kifuani, RPC Mkumbo anasema Mbise amejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwili wake. Sasa hapa tumuamini nani? Mbise au RPC? I smell something fishy.!
Tatu ni hujuma kwa viongozi wa Chadema. Wa kwanza ni Innocent Kisanyage, Katibu wa Chadema Arusha. Huyu hakuwepo eneo la vurugu juzi. Alisikia tu kwamba kuna wafuasi wa Chadema wamekamatwa, akiwa kama kiongozi akaenda ili kuona ni jinsi gani anaweza kuwasaidia. Alipofika naye akakamatwa na kuwekwa rumande, ambapo hajatoka hadi leo.
Hivi unamkamataje mtu ambaye hakuwa kwenye premise ya tukio? Je kuna ushahidi wowote kwamba labda yeye ndiye aliyewatuma wafuasi wake wamfanyie fujo Mbise? Kama hamna kwanini amekamatwa?
Siku ya 3 sasa Kisanyage analala rumande wakati yeye ndiye mratibu wa kampeni katika kata zote zinazorudia uchaguzi Arusha mjini. Maana yake ni kwamba shughuli za uratibu zimesimama kwa sababu mratibu hayupo. Nadhani lengo hapa ni zaidi ya Mbise kupigwa teke.
Wa pili ni Mhe.Lema kuhujumiwa. Nimetumiwa "conversation" ya group la whatsaap inayoonyesha baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM mkoani Arusha wakishinikiza jeshi la polisi limkamate Lema na kumuunganisha katika kesi hiyo. Nikajiuliza Lema aunganishwe kama nani? mtuhumiwa, shahidi upande wa walalamikiwa au shahidi wa jamhuri?
Ajabu ni kwamba wakati tukio hilo linatokea Lema wala hakuwepo Arusha. Alikuwa Moshi kwenye kikao fulani na baadhi ya viongozi waandamizi wa serikali na viongozi wa dini. Sasa anaunganishwaje kwenye hiyo kesi? CCM ni wavivu kufikiri hadi wanakera.
Asubuhi ya siku ya tukio Lema alianzia ofisini kwake kwenda kuratibu ugawaji wa fedha za mfuko wa jimbo, kisha akaenda Ngome ya chama pale Kwa Mrombo, then mchana akaenda Moshi kwenye kikao hicho nyeti kilichoshirikisha baadhi ya viongozi wakuu wastaafu wa taifa hili. Akiwa Moshi ndipo vurugu zikatokea Arusha. Sasa viongozi wa CCM wanaposema aunganishwe kwenye kesi, wanamaanisha nini? This is non sense. Nitalishangaa sana jeshi la polisi likifuata ushauri huu wa viongozi hawa "mandondocha"
CCM please try to be smart even a little bit. Mnakuwa outsmarted na vitu vidogo mno hadi mnadhalilika bila sababu. Siku hizi unaweza kujua mtu alipo kwa kutrack simu yake kuppitia CL sites. Mngekuwa makini kabla hamjapayuka Lema aunganishwe kwenye kesi, mngepeleleza kwanza simu yake kusoma CL site, ili mjue wakati tukio linatokea alikuwa wapi. Mngeona imesoma Moshi wala msingehangaika.
Lakini kwa ujinga wenu wa kiwango cha shahada ya uzamivu, mmeamua kujidhalilisha hadharani. Mnaonesha msivyo smart hata kidogo.
Niwaeleze tu kwamba Lema hana wasiwasi hata kidogo. Akiitwa polisi ataenda na ushahidi wa mawasiliano yake ya siku hiyo ambayo CL sites zinasoma Moshi. However kama ikibidi, basi baadhi ya viongozi waliokuwa na Lema (wengine ni mawaziri wastaafu na viongozi wa dini), watakuwa sehemu ya ushahidi kuthibitisha kwamba siku na muda ambao tukio hilo linatokea Arusha walikuwa naye Moshi.
Kutokana na trende ya suala hili lilivyo, huenda tukio hili la kupigwa kwa Mbise ni mkakati maalumu wa kuwazorotesha Chadema washindwe kucocentrate na kampeni. I smell malice aforethought behind the saga. Ndio maana CCM wanashinikiza Lema akamatwe. Waanajua akikamatwa atasumbuliwa kwa siku kadhaa mahabusu, akija kuachiwa kampeni zimeisha. Na kwa kuwa Katibu wake yupo rumande basi CCM wanaamini Chadema itashindwa kujiratibu kwenye kampeni.
Bahati mbaya walichosahau ni kwamaba mbinu hizo ovu hazitawasaidia kupata kura. Hizi nguvu wanazoziwekeza kuhujumu Chadema, wangeziwekeza kwa wananchi kuomba kura pengine wangewafikiria. lakini kwa haya wanayofanya wanazidi kujiharibia.!
Malisa GJ
No comments:
Post a Comment