Kahawa (Coffee) ni kinywaji Cha tatu kinachonyweka zaidi Duniani baada ya maji na chai. Na kama ulikuwa hujui pia ni Kuwa Kahawa ni bidhaa ya pili inayouzwa zaidi Duniani (Most traded commodity) baada ya Mafuta (Crude Oil).
Nchi maarufu Kwa uuzaji kahawa Duniani ni Brazil ikifuatiwa na Vietnam.
Kwenye Kumi Bora zinaingia nchi mbili tu za Africa ambazo ni Ethiopia yenye uwezo wa kusafirisha metric tones 384,000 ikishika nafasi ya Tano kidunia na Uganda yenye uwezo wa kusafirisha na kuuza metric tones 288,000.Mwaka 2019 Kenya walifanikiwa kuuza Kahawa yenye thamani ya USD 224 Milioni na kwa mwaka huo Kahawa ilikuwa ni zao la nne kwa kuuzaa nje ya nchi Kenya huku ikishika nafasi ya 25 Kwa kuuza Kahawa nje ya nchi yao kidunia.
Magendo na Urasimu
Mwaka 2018 Gazeti la Mwananchi liliripoti kuwa Burundi imeishangaza Dunia Kwa kuuza Kahawa nyingi Sana Duniani. Ukweli ni kwamba wakulima wengi wa mipakani Tanzania huuza Kahawa yao Kwa magendo Uganda na Burundi Kwa kuwa Kuna Bei nzuri.
Kwa Bei ya Sasa Kilo Moja ya Uganda Kahawa iliyokobolewa (Bean) ni Shilingi 12,000 Kwa Tanzania ni Shilingi 7,000. Hii inachochea watu kutorosha kahawa kupeleka huko Uganda.
Nafikiri Wizara ya Kilimo itoe Mwongozo kuwa Mtu binafsi anaweza kuuza Kahawa yake nje ya nchi Moja kwa Moja bila kuzuiwa. Wananchi wengi hawajui Soko la bidhaa hii adhimu lipoje. Kama wakulima wetu wakisaidiwa kupeleka kahawa yao Sokoni bila vizingiti na Urasimu wa kulazimishwa kuwauzia Madalali au Vyama vya Ushirika basi wananchi watakuwa matajiri.
Uganda inaingiza Fedha nyingi Sana kwenye Kilimo hiki. Hatuna sababu ya kukwama na kuanza kumfukuza Mkulima wa kahawa na kahawa yake kama amebeba bangi. Balozi zetu huko nje zinaweza kusaidia hili Sana kuonyesha masoko yapo wapi ili wananchi wetu wanufaike.
Wizara ya Kilimo na Wizara ya Biashara iwe na Dawati Moja la kusaidia Hawa wakulima Kwa kutoa Elimu ya kahawa Bora na kuwasaidia kuwatafutia Soko.
Leo Bei ya kahawa ambayo haijakobolewa Kagera ni 1,100 Kwa Kilo lakini Mkulima akiivusha tu hapo Uganda anapata 3,000 Kwa Kilo. Kwa kuwa wanaifanya Kwa magendo wanalazimika wengine kuzama majini wakiwa wanavusha.
Serikali iruhusu sector binafsi inunue Kahawa na Mkulima aruhusiwe kuuza popote anapotaka
No comments:
Post a Comment