Translate

Monday, February 29, 2016

JESHI LA POLISI ZANZIBAR LATOA UFAFANUZI KUHUSU KUMKAMATA MAALIM SEIF SHALIF HAMAD

Jeshi la Polisi Zanzibar limetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zinazosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa jeshi hilo linapanga kumkamata Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi, CUF, Maalim Seif Sharif Hamad.


Taarifa zinazosambaa kwa kasi mitandaoni  zinasema Maalim Seif anatakiwa kukamatwa kwa tuhuma zinazohusiana na kujitangazia ushindi katika uchaguzi wa tarehe 25 Oktoba 2015 kama inavyoshinikizwa na Chama cha Mapinduzi Zanzibar.

Akiongea  na mwandishi wa Dw, Issac Gamba, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Kamishina Mkadam Khamis Mkadam, amesema yeye hajapata taarifa yoyote toka kwa wakubwa wake inayomtaka amkamate Maalim Seif.

Amesema jeshi la polisi ni taasisi kubwa inayohusisha viongozi mbalimbali, hivyo yaweza  kuwa amri kama hiyo imetolewa kwa viongozi wengine

No comments:

Post a Comment