Translate

Monday, February 8, 2016

MSEKWA : JK ONDOKA NA MUUNDO WAKO



Siku moja baada ya CCM kuadhimisha miaka 39 tangu kuzaliwa kwake, kada mkongwe na muasisi wa chama hicho, Pius Msekwa amesema kuna haja ya kufanya mabadiliko ndani ya chama hicho hasa muundo wa halmashauri kuu ya taifa.

Katika chapisho lake kuhusu tathmini ya miaka 39 ya chama hicho itakayochapwa kesho na gazeti la Mwananchi, Msekwa amesema mabadiliko hayo yanahitajika kufanywa kabla ya mwenyekiti wa sasa wa CCM, Rais mstaafu Jakaya Kikwete kukabidhi kijiti hicho kwa Rais John Magufuli.

No comments:

Post a Comment