Rekodi ya video ya muziki iliyotazamwa na watu wengi kwa muda mfupi kwenye mtandao wa Youtube nchini Tanzania iliyokuwa inashikiliwa na video ya wimbo wa Salome wa Diamond Platnumz, imevunjwa na video ya wimbo mpya wa Alikiba ‘Seduce Me’.
Video ya wimbo wa Salome ilitazamwa na watu milioni 1 kwa siku mbili huku video mpya ya Seduce Me imetumia masaa 37 yaani siku moja na masaa 13 kufikisha views milioni 1 na kuweka rekodi ya video iliyotazamwa zaidi kwa muda mfupi Tanzania na Afrika Afrika mashariki kwa ujumla.
Kwa sasa video inayoongoza kushikilia rekodi ya kutazamwa zaidi kwa muda mfupi barani Afrika baada ya kutoka ni Video ya Closer ya Wizkid ambayo ilitazamwa na watu milioni 1 kwa masaa 23.
Hata hivyo bado video ya Salome inashikilia rekodi ya video iliyotazamwa zaidi ndani ya wiki moja kwa kufikisha watazamaji milioni 3.
Je, kwa mwendo huo video ya ‘Seduce Me’ yenye siku mbili tangia itoke na tayari imetazamwa mara milioni 1.2 itavunja rekodi ya ‘Salome’ kutazamwa mara milioni 3 kwa siku 7?
No comments:
Post a Comment